God Plan ya Drake kileleni chati za Billboard.

Written by on February 2, 2018

Rapper kutoka Toronto, Drake ametinga katika chati za muziki za Billboard Hot 100 kupitia ngoma yake mpya ya ‘God Plan.

Ngoma hiyo ya ‘ God Plan’ ilitoka mwezi Januari mwaka huu katika Mixtape yake ya ‘Scary Hours’. Wakati ‘God Plan’ ikishika namba moja ngoma ya ‘Perfect’ kutoka kwa Ed Sheeran na Beyonce ikiwa namba mbili huku namba tatu ikiwa imeshikiliwa na Camila Cabello kupitia ngoma yake ya ‘Havana’ aliyomshilikisha rapper Young Thug.

Namba nne kwa wiki hii kupitia chati za Billboard Hot 100 imeshikiliwa na Post Malone kupitia ngoma ya ‘Rockstar’ aliyomshirika rapper 21 Savage, naye mshindi wa tuzo za Grammy 2018 toleo la 60 Bruno Mars ambaye alinyakuwa tuzo 6 akiwa anashikilia namba tano katika chati za Billboard Hot 100 kupitia ngoma yake ya ‘Finesse’ aliyomshirikisha mwanadada Cardi B.

 


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


Continue reading

Clouds FM

The People's Station

Current track
TITLE
ARTIST

Background