Trump Awapatia Maelfu ya Wakimbizi Kutoka Syria Ruhusa Kuishi Marekani

Written by on February 2, 2018

Serikali ya Rais Donald Trump imeongeza kinga ya muda kwa karibu wakimbizi 7,000 wa Syria wanaoishi nchini Marekani wakati vita vikiendelea nchini mwao.

Walikuwa wamepewa kinga ya muda dhidi ya ya kurejeshwa nyumbani chini ya mpango wa kibinadamu unaofahamika kama –Temporary Protected Status (TPS).

Rais Trump amefuta mpango huo kwa nchi mbali mbali katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni, na hivyo kuwaathiri wahamiaji kutoka kutoka El Salvador, Haiti na Nicaragua.

Marekani ilisema kuwa haitakubali maombi ya wahamiaji kupitia TPS kutoka Syria.

“Ni wazi kwamba hali iliyoyopelekea Syria kuchaguliwa ina msingi wa kuendelea kuwepo, kwa hivyo kurefushwa kwa muda wa kinga kwa wakimbizi kunakubalika chini ya sheri ,” alisema waziri usalama wa ndani Kirstjen M Nielsen katika taarifa yake.

“Tutaendelea kuchunguza maombi ya kila nchi kwa kuzingatia hali ya nchi husika. Kwa raia wa Syria ambao tayari wanaishi na kufanyia kazi nchini Marekani, mpango wa TPS utarefushwa kwa miezi mingine 18. Lakini Wasyria walioingia nchini Marekani baada ya Agosti 2016 watatengwa na mpango huo licha ya kuendelea kwa hali mbaya nyumbani.”


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


Clouds FM

The People's Station

Current track
TITLE
ARTIST

Background