Wachimba Mgodi 955 Waliokwama Afrika Kusini Waokolewa

Written by on February 2, 2018

Wachimba mgodi wote 955 waliokuwa wamekwama katika mgodi mmoja wa dhahabu ulioko mkoa wa Free State nchini Afrika Kusini wameokolewa wakiwa salama.

Walikuwa wamekwama ndani ya mgodi huo baada ya umeme kukatika Jumatano usiku.

“Kila mtu ametolewa,” James Wellsted, msemaji wa kampuni inayosimamia shughuli kwenye mgodi huo ya Sibanye-Stillwater amesema.

Ameeleza kuwa kuna visa kadha vya “watu kupungukiwa na maji mwilini na shinikizo la damu, lakini hakuna aliye na tatizo kubwa.”

Mgodi huo wa dhahabu wa Beatrix unapatikana kilomita 300 Kusini Magharibi mwa Johannesburg na una ngazi 23 ambapo hufika hadi mita 1,000 chini ya ardhi.

Chanzo cha wachimba migodi hao kukwama ilitokana na mvua kubwa iliyonyesha nyakati za usiku wakati wachimba migodi hao walipokua chini ya mgodi huo na kuangusha nguzo ya umme iliyosababisha umeme kukatika

Afrika Kusini inaongoza kwa uchimbaji wa madini lakini usalama katika migodi umekuwa wa kutiliwa shaka.


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


Clouds FM

The People's Station

Current track
TITLE
ARTIST

Background