Mtoto ‘Ombaomba’ apata msaada wa kusomeshwa.

Written by on February 6, 2018

Jana kwenye kipindi cha #PowerBreakFast ilisikika stori ya mtoto Mussa (Sio jina lake halisi} ni mwanafunzi wa darasa la nne katika shule moja hapa nchini, amekuwa akionekana maeneo ya Kariakoo na Posta akiombaomba, wazazi wake wote wamefariki anaishi na bibi yake ambaye hana uwezo wa kumuhudumia, mtoto huyu ana uwezo mkubwa darasani lakini inamlazimu aingie mitaani kuomba misaada ili amsaidie Bibi yake.

Baada ya taarifa hii kusikika jana, watu wengi waliguswa ili waweze kumsaidia mtoto huyu, uongozi wa shule ya Oasis English Medium imejitokeza kumsomesha hadi amalize elimu yake ya msingi, na baada ya kumaliza wataangalia utaratibu mwingine kutokana na uwezo wake darasani.

Meneja wa shule hiyo, Hassan Juma Kombo ameweka wazi utaratibu wa kumpokea mtoto huyo shuleni hapo.

‘’Tunafanya utaratibu ili tuweke kumpokea mtoto Mussa hapa shuleni, tutamsomesha elimu yake yote ya msingi na baada ya kumaliza tutaangalia utaratibu mwingine kutokana na uwezo wake darasani’’ Alisema Hassan Kombo..

 


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


Continue reading

Clouds FM

The People's Station

Current track
TITLE
ARTIST

Background