Dogo janja hataki kupanda Mlima Kilimanjaro, Uwoya atosha.

Written by on February 9, 2018

Msanii Dogo Janja asubuhi ya leo amefanya mahojiano na kipindi cha 360 cha Clouds Tv na kusema kuwa hataki kupanda Mlima Kilimanjaro, wala hataki kwenda Serengeti.

“Sitaki kupanda Mlima Kilimanjaro wala sitaki kwenda Serengeti kwa sababu nina KITU cha kitalii NDANI” Janjaro.

Pia Dogo Janja amesema kuwa alivyokuwa mdogo alikuwa anakata vipande vya magazeti anabandika ukutani.

Picha alizokuwa anaweka ni za mkewe Irene Uwoya, Baba yake alikuwa anamind sana lakini Dogo anasema hiyo ni kwa sababu alikuwa anamtamani Uwoya tangu kitaambo.

Kwa mara ya kwanza alikutana na Uwoya kwenye birthday ya Uwoya ambapo alienda bila kualikwa na akaamua kuimba bure.

Anamzungumziaje Aslay?

Dogo Janja amesema anachokipenda kwa msanii mwenzake Aslay ni kwamba muziki wake unagusa matabaka yote

“Yule anagusa kuanzia watu wa maisha ya chini kabisa mpaka wa juu wanamkubali”. Pia anasema watu wamezoea kumuona akiimba ‘playback’ lakini hawajui kwamba ni mkali sana akiimba live. ” Yule ni vocalist, akiimba live ni mbaya sana.

#MapenziMubashara18: Feb 17 @aslayisihaka anapiga live, mshkaji wake Dogo Janja anamuangalia kutokea VIP akiwa na Uwoya.


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


Clouds FM

The People's Station

Current track
TITLE
ARTIST

Background