Ndege kugeuzwa kuwa mgahawa yawa kivutio, Ethiopia.

Written by on February 9, 2018

Mjasiriamali wa Addis Ababa,nchini Ethiopia, Guttama Gutta amenunua ndege mbovu ambayo haitumiki kubeba abiria aina ya Boeing 737 na kuigeuza kuwa mgahawa.

Mwekezaji huyo alitumia dola mill. ($ 73,000,000) kununua ndege hiyo, kurekebisha na kuipamba , alitumia miaka 2 kufanya marekebisho ya  “hoteli hiyo mpya ya ndege” iliyopo kwenye mji wa Burayu, kilomita 15km magharibi mwa mji mkuu wa Addis Ababa.

Alipoulizwa kwa nini alianzisha mgahawa wa ndege katika mji huo, alielezea kuwa nia yake ilikuwa ni kuboresha biashara yake ya awali na kwa kufanya hivyo biashara ya ndege ilikuja.

Pia aliongeza kuwa alifanya uwekezaji kwa matumaini ya kujenga kituo cha burudani katika Burayu.


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


Continue reading

Clouds FM

The People's Station

Current track
TITLE
ARTIST

Background