Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amepewa saa 48 kujiuzulu.

Written by on February 13, 2018

Kwa mujibu wa taarifa ya shirika la Utangazaji la Afrika Kusini -SABC- na vyanzo vingine vya habari, hatua ya kumtaka Rais Zuma ajiuzulu inakuja baada ya mlolongo wa mazungumzo yaliyofanywa na chama tawala nchini humo (ANC).

Duru zinasema ANC kilifanya mazungumzo marefu baadaye kuwatuma watu wawili nyumbani kwa Rais Zuma jijini Pretoria kwenda kumfikishia ujumbe wa chama ana kwa ana ya kwamba Zuma ajiuzulu mwenyewe au chama kimng’oe madarakani.

Lakini haijulikani bado kwamba Rais Zuma alipokeaje ujumbe huo.

Hatua hii ya ANC inaonekana ndio njia rahisi zaidi ya chama hicho kumng’oa rais Zuma madarakani badala ya kusubiri utaratibu wa bunge ambao ungeweza kuwa mrefu na wenye madhara zaidi kwa chama cha ANC.

Rais Jacob Zuma ambaye anakabiliwa na mashtaka kadhaa ya rushwa, alishindwa uongozi wa chama tawala Desemba mwaka jana.

Kiongozi mpya wa ANC, Cyril Ramaphosa anaongoza shinikizo za kumuondoa Zuma katika nafasi yake hiyo ya Urais, na hatimaye kushika pia nafasi hiyo.

Ramaphosa ameahidi pia kupambana na rushwa iliyokithiri na kukijenga upya chama cha ANC, wakati nchi hiyo ikielekea katika uchaguzi mwakani.

Chanzo BBC

 


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


Continue reading

Clouds FM

The People's Station

Current track
TITLE
ARTIST

Background