Mkuu ya wilaya ya Kisarawe aelezea mikakati ya kukomesha mimba za utotoni kwenye wilaya yake.

Written by on February 15, 2018

 

Asubuhi ya leo kupitia #PowerBreakFast, Mkuu wa wilaya ya Kisarawe, Happiness Seneda ameelezea kusikitishwa kwake baada ya wilaya hiyo kuongoza kwa mimba za utotoni, ambapo ameelezea mikakati ya kupunguza tatizo hilo au kulikomesha kabisa.

“Tatizo hili lipo zaidi kwa wanafunzi wa shule za msingi hasa darasa la saba, mkoa wa Pwani una halmashauri tisa kati ya hizo wanafunzi 14 walipata ujauzito, ni tatizo kubwa”

“Sheria ya nchi inasema kama ikithibitishwa na mahakama kuwa mwanaume akimpa mimba mtoto (chini ya miaka 18) atahukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, lakini changamoto kubwa ipo kwenye jamii wengi wanaogopa kuwafunga watuhumiwa wakihofia malezi ya mtoto atakayezaliwa, tunapambana sana”

“Mikakati tulionayo ili kukomesha tatizo hili tunatafuta ‘resources’ kwa ajili ya kipata hostel kwa wanafunzi wa kike” Happiness Seneda.


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


Clouds FM

The People's Station

Current track
TITLE
ARTIST

Background