Rais wa FIFA: Tanzania ni nchi ya soka

Written by on February 23, 2018

 

Rais wa Shirikisho la Soka la duniani (FIFA) Gianni Infantino, akiwa nchini Tanzania kuhudhuria mkutano wa shirikisho hilo nchini.

Mkutano huo ulishirikisha jumla ya mashirikisho 21 ya kandanda ambao ni wanachama wa shirikisho hilo.

Rais wa shirikisho hilo la soka duniani alikutana na Waziri Mkuu wa nchi , Kassim Majaliwa pamoja na Waziri wa Utamaduni na Michezo Harryson Mwakyembe.

Katika mkutano na waandishi wa habari, Bw Infantino amesisitiza kuzungumzia hali ya rushwa katika mpira wa miguu.

“Tumefanikiwa sana katika kuweka uwazi wa matumizi ya fedha za FIFA. Leo FIFA ni shirikisho lenye uwazi. Tunachapisha matumizi ya fedha zote. Kila mtu anaweza kufuatilia fedha zinatoka wapi na fedha zinaenda wapi.”


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


Clouds FM

The People's Station

Current track
TITLE
ARTIST

Background