Chege: Nitakuwa wa mwisho kuoa.

Written by on February 26, 2018

Chege Chigunda ni msanii pekee wa Bongo Fleva ambaye ameendelea kushikilia rekodi ya kuwa na nidhamu kwenye kazi yake hasa kwenye suala la ‘Mahusiano’ amekuwa msiri mno… Siku za hivi karibuni baadhi ya wasanii wamefunga ndoa, yeye ana mpango gani?

“Huwa sipendi kuambiwa nifanye kitu ambacho mwingine amekifanya, nina mpenzi ninayempenda kabisa na tunaishi pamoja, muda ukifika nitaoa, ninachogundua nitakuwa wa mwisho kuoa” Chege ameyazungumza hayo kwenye kipindi cha Leo Tena leo wakati akitambulisha ngoma yake ya Kaitaba aliyomshirikisha msanii Saida Karoli.


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


Clouds FM

The People's Station

Current track
TITLE
ARTIST

Background