Simalenga awaomba wadau wa elimu kuchangia shule ya Tengero..

Written by on February 26, 2018

Simon Simalenga, Afisa Uhusiano wa Clouds Media Group, Leo amezungumza na Power Break Fast kufikisha ujumbe kwa wadau mbalimbali wa elimu ili kujitolea kuchangia shule ya msingi aliyosoma ya Tengero iliyopo Kata ya Langali, wilayani Mvomero, mkoani Morogoro.

“Hivi karibuni nilitembelea shule ya msingi niliyosoma, sasa hivi tunaonekana watu wa aina fulani lakini wapo watu waliotufundisha (walimu) ndio waliotufanya tuonekane tulivyo hivi sasa, nimeikumbuka shule yangu niliyosoma ya Tengero, nilikwenda kujionea maendeleo, lakini nilichokikuta nimeshindwa kujizuia ndio maana nikaona niwatafute wadau muhimu wa maendeleo kwenye sekta zote ili waweze kuisaidia hii shule vifaa mbalimbali kuanzia ujenzi wa shule na mahitaji mengine” @official_simalenga

Kwa maelezo zaidi kutoka kwa Simalenga piga namba hii 0686066006


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


Clouds FM

The People's Station

Current track
TITLE
ARTIST

Background